Vifo vya IDAI vinaongezeka , huku mlipuko wa kipindupindu waongeza hofu Msumbiji:OCHA

April 1, 2019

Umoja wa Mataifa Msumbiji tayari unawasaidia walioathirika na mafuriko yaliyotokana na kimbunga IDAI

 

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA , idadi ya vifo vilivivyosababishwa na athari za kimbunga Idai nchini Msumbiji imeongezeka na kufikia 493.

 

Shirika hilo linasema mlipuko wa kipindupindu ulioripotiwa katika eneo la Nhamatande umeongeza tishio ingawa tayari vituo 9 vya matibabu vimeanzishwa kwenye jimbo la Beira na maeneo mengine.

 Hadi sasa watu 140,000 wametawanywa katika maeneo 161 kwenye majimbo ya Sofala, Manica, Zambezia, na tete na 7400 kati yao wameelezewa kuwa wako hatarini na wasiojiweza kwa mujibu wa serikali..

 

Mashirika ya Umoja wa mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF, la afya WHO, la mpango wa chakula WFP na mashirika mengine ya kimataifa kama COSACA na World Vision yametoa taarifa ya pamoja kuhusu lishe kwa watoto wachanga katika juhudi za kukabiliana na hali nchini Msumbiji.

 

 

Wadau wa afya wanajikita katika kuimarisha ufuatiliani wa magonjwa na kudhibiti mlipuko wa kipindupindu.

 

Maaandalizi ya chanjo ya kipindupindu iliyopangwa kuanza wiki ijayo yanaendelea huku vituo tisa vya matibabu vimeanzisha na saba kati ya vituo hivyo tayari vimeanza kufanya kazi vikiwa na takribani vitanda 400

 

Wakati huohuo kwenye jimbo la Manica ongezeko la visa vya malaria limeripotiwa katika wilaya mbalimbali na hatari ya mlipuko wa kipindupindu ni kubwa katika wilaya nyingi zilizoathirika na Idai.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon