Kundi la Taleban laanzisha operesheni kali ya kuangamiza ngome za genge la Daesh (ISIS) mashariki mw


Kundi la Taleban limeanzisha operesheni ya mashambulizi makali dhidi ya ngome za genge la kigaidi la Daesh (ISIS) mashariki mwa Afghanistan.

Taleban imeanzisha operesheni hiyo ya kuwasambaratisha wanachama wa kundi hilo linaloungwa mkono na Marekani, baada ya kusimamia mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani ambapo zilianza Alhamisi ya jana katika miji ya Chapa Dara na Manogi katika jimbo la Kunar nchini humo.

Katika operesheni hizo makumi ya wanachama wa kundi la Daesh wameripotiwa kuuawa hadi sasa na wengine kujeruhiwa.

Khalilullah Khalili, mkuu wa wilaya ya Chapa Dara amesema kuwa, mamia ya familia za wakazi wa eneo hilo wamelazimika kuyakimbia makazi yao kufuatia mapigano makali kati ya wanachama wa Taleban na Daesh.

Makundi ya Daesh na Taleban ambayo licha na kuwa na idolojia moja, lakini ni mahasimu wakubwa

Inafaa kuashiria kuwa, baada ya kundi la Daesh (ISIS) kushindwa vitani na wapiganaji wa Taleban katika mkoa wa Nangarhar, lilijaribu kuhamishia shughuli zake katika majimbo mengine ya mashariki mwa Afghanistan.

Hata hivyo kundi la Taleban limekuwa likizuia kusonga mbele kwa genge hilo ambalo wanachama wake wamehamishiwa nchini humo na askari wa Marekani kutoka nchi za Syria na Iraq.

Hii ni katika hali ambayo Marekani imekuwa ikifanya mashambulizi yake makali ya anga dhidi ya wapiganaji wa Taleban kwa ajili ya kuwazuia kulisambaratisha kundi la Daesh.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu