Ugonjwa wa TB waua watu 4,500 kila siku, WHO yaazimia kuutokomoeza


Ugonjwa wa kifua kikuu au TB huua watu 4,500 kila siku duniani na Shirika la Afya Duniani WHO, limeazimia kutokomeza ugonjwa huo sugu.

Kwa msingi huo, katika kuelekea siku ya kifua kikuu itakayoadhimishwa tarehe 24 mwezi huu WHO imetoa mwongozo mpya wa jinsi ya kuboresha matitabu ya ugonjwa huo wa kifua kikuu.

Katika taarifa ya jana Jumatano WHO inasema matibabu mapya ni bora zaidi na yana kiwango kidogo cha kuweza kusababisha madhara ya baada ya matumizi.

Pia shirika hilo linapendekeza matumizi ya dawa hizo kwa kufuata usalama wa dawa na pia kuwasaidia wagonjwa na kuwapa ushauri wa kuwasaidia kumaliza dozi ya matibabu yao.

Mapendekezo haya mapya , ni sehemu ya mkusanyiko wa hatua zilizoandaliwa ili kusaidia nchi kuongeza kasi katika maendeleo ya kutokomeza TB.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, “kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya TB duniani :” Ni wakati wa kukikotokomeza Kifuu Kikuu,Tunasisitiza umuhimu wa kutekeleza ahadi zilizofikiwa mwaka 2018 katika mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kifua Kikuu katika kuchukua hatua za kuhakikisha kila mmoja anayehitaji matibabu ya kifua kikuu anayapata.”

Taarifa ya WHO inayopatikana pia katika tovuti ya shirika hilo inasema tangu mwaka 2000, maisha ya watu wapatao milioni 54 yameokolewa na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kifua kikuu vimepungua kwa theluthi moja. Lakini inaendelea kufafanua kuwa bado watu milioni 10 wanaugua kifua kikuu kila mwaka.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu