Utafiti: 25% ya wananchi wa Ulaya wanatamani kuongozwa na maroboti badala ya wanasiasa


Utafiti mpya wa maoni umefichua kuwa, zaidi ya robo ya wananchi wa Ulaya wangependa maamuzi muhimu ya nchi zao yachukuliwe na maroboti badala ya viongozi wa kisiasa waliowachagua wao au watumishi wa umma walioteuliwa.

Utafiti huo uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Chuo Kikuu cha IE cha Uhispania (Center for the Governance of Change) umesema kuwa, katika kila raia wanne wa Ulaya, mmoja anatamani maroboti yaendeshe masuala muhimu ya nchi yake, kulikoni viongozi wao wa kisiasa (binadamu).

Kwa mujibu wa utafiti huo, kiwango hicho cha wananchi wa Ulaya wa matabaka yote, katika elimu, jinsia, na mirengo yote ya kisiasa kufadhilisha kuongozwa na maroboti, ni ishara ya kuchoshwa na maafisa na viongozi wao.

Takwimu za Center for the Governance of Change

Mkurugenzi wa kituo hicho cha utafiti cha Uhispania, Diego Rubio amesema kuwa, utafiti huo umefichua kuwa wananchi wa Ulaya wanatilia shaka au hawaridhishwi na mfumo wa uwakilishi katika demokrasia ya nchi zao.

Asilimia 43 ya wananchi wa Uholanzi wanaunga mkono wazo hilo kwamba, maamuzi mahimu ya nchi yao yanapaswa kuchukuliwa na maroboti yenye intelijensia bandia, badala ya viongozi wao wanadamu, ikifuatiwa na Ujerumani na Uingereza zote asilimia 31.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu