Wimbi la kujiua watu mashuhuri nchini Marekani laongezeka, wa karibuni kabisa ni Mshauri Mkuu wa uch


Watu mashuhuri waliojiua Marekani hivi karibuni. Ingawa nyuso zao zina bashasha lakini inaonekana majonzi na kukata tamaa kuligubika nyoyo zao.

Alan Krueger, mkuu wa baraza la washauri wa kiuchumi wa serikali ya zamani ya Marekani na ambaye ni mmoja wa wanauchumi bora na maarufu duniani, amejiua

Kwa mujibu wa gazeti la Financial Times, familia ya Alan Krueger (58) imethibitisha kuwa sababu ya kifo chake kilichotokea wiki iliyopita ni kujiua.

Mhadhiri huyo maarufu wa Chuo Kikuu cha Princeton alikuwa mmoja wa washauri muhimu wa Ikulu ya Marekani, White House,

wakati wa serikali ya Barack Obama. Hata kabla ya kuanza kazi rasmi katika ikulu hiyo, Krueger aliisaidia Marekani kutoka katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi wa mwaka 2008.

Hata wakati wa Bill Clinton, rais wa zamani wa Marekani, Krueger alikuwa miongoni mwa wanauchumi wakubwa katika Wizara ya Kazi ya nchi hiyo

Alan Krueger amejiua katika hali ambayo alikuwa anahesabiwa kuwa ni mmoja wa wanauchumi 50 bora zaidi duniani. Habari ya kujiua kwake ghafla imetolewa katika hali ambayo wiki iliyopita yaani wiki hiyo hiyo aliyojiua alitoa hotuba muhimu katika Chuo Kikuu cha Princeton kuhusiana na mapato ya watu na soko la ajira.

Katika miaka kadhaa ya hivi karibuni watu wengi maarufu wamejiua huko Marekani akiwemo Scott Stearney, kamanda wa wanajeshi wa Marekani walioko Bahrain, Robin Williams, mcheza filamu maarufu wa Hollywood, Anthony Bourdain, mmoja wa watangazaji maarufu wa televisheni ya CNN na Kate Spade mmoja wa wanamitindo wakubwa nchini Marekani.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu