Ajali ya treni yaua na kujeruhi zaidi ya watu 130 DRC


Ajali ya garimoshi la kusafirishia mizigo iliyotokea siku ya Jumapili katika mkoa wa Kasai wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesababisha kupoteza maisha zaidi ya watu 50 na kujeruhiwa wengine wapatao 80.

Mabehewa,garimoshi na reli zinazopita garimoshi hizo zimechakaa mno huko DRC kwani ni zile za tangu enzi za ukoloni, kabla ya kupata uhuru nchi hiyo tajiri kwa maliasili ya katikati mwa Afrika.

Hali ya usafiri katika nchi hiyo kiujumla ni mbaya mno kiasi kwamba wananchi wanalazimika kudandia hata magarimoshi mabovu na yaliyochakaa ya mizigo ili kufika wanakokwenda.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu