Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Wanawake kutokuwa na sauti kunachochea ndoa za utotoni na ukeketaji Kajiado, Kenya- Bi. Parit

March 19, 2019

Sevirina Sangurikuri, mmoja wa wanawake wanaohudhuria mkutano wa 63 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW63, kutoka jamii ya watu wa asili ya Samburu nchini Kenya.

 

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake kikao cha 63 unaendelea mjini New York, Marekani ambapo vikao mbali mbali vinafanyika katika kupaza sauti za wanawake na kujadili changamoto wanazokabiliana nazo lakini pia jinsi ya kuzitatua.

 

Suala la ndoa za utotoni ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazozikabili jamii nyingi  na huku Umoja wa Mataifa usisitiza tatizo hilo lililomea mizizi na kuwa kama donda ndungu lazima likomeshwe kabla ya waka 2030.

 

Hivi sasa serikali, jamii na hata wanaharakati wameamua kulivalia njuga suala hilo.

 Mmoja wa wanaharakati hao ni mwanamke Dorcus Parit mwanzilishi na mkurugenzi wa  kituo cha mpito cha Hope Beyond huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambacho ni kimbilio kwa wasichana wanaoingizwa kwenye ndoa za utotoni au wale wanaokabiliwa na hatari ya kukeketwa. 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload