Raia 10 wa Syria wauawa katika mashambulizi ya ndege za muungano vamizi


Duru za habari za Syria zimetangaza kuwa raia kumi wa nchi hiyo wamuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na ndege za muungano vamizi unaoongozwa na Marekani huko mashariki mwa Syria.

Raia wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyofanywa na ndege za kivita za muungano huo eti wa kupambana na kundi la kigaidi la Daesh unaoongozwa na Marekani. Ndege hizo zimefanya mashambulizi hayo katika kambi ya al Baghuz mashariki mwa mkoa wa Deir- Zor nchini Syria.

Katika miaka ya karibuni, Marekani imekuwa ikifanya mauaji dhidi ya raia wa Syria katika mashambulizi yake yanayofanyika kwa kisingizio cha kupambana na Daesh.

Katika upande mwingine, jeshi la Syria limezishambulia kambi za magaidi katika oparesheni zilizofanywa na jeshi hilo katika vijiji vya al Shari'a na al Twina katika mkoa wa Hama na kuangamiza idadi kadhaa na magaidi hao wa kitakfiri.

Oparesheni ya jeshi la Syria dhidi ya magaidi katika mji wa Hama.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, makundi kadhaa ya kigaidi yapo katika vitongoji na vijiji vya kaskazini mwa mji wa Hama mkoani Idlib.

Magaidi wengi wa makundi hayo ya kitakfiri yanayoungwa mkono na kufadhiliwa na Marekani, Saudi Arabia, Israel na washirika wao wameangamizwa katika oparesheni nyingi za jeshi la Syria.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu