Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mafuriko yaendelea kuua katika nchi za kusini mwa Afrika

March 15, 2019

Makumi ya watu wamepoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Malawi.

 

Chipiliro Khamula, Msemaji wa Idara ya Kupambana na Majanga nchini humo amesema watu zaidi ya 56 wamepoteza maisha kutokana na janga hilo, huku wengine zaidi ya 600 wakijeruhiwa.

 

Kadhalika watu 83,000 wameachwa bila makazi kutokana na mvua kubwa zilizoyakumba maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.

 

Haya yanajiri huku watu wasiopungua 66 wakipoteza maisha na laki moja na 41 elfu wakiathirika kutokana na mvua kubwa zilizoyakumba maeneo ya katikati na kaskazini mwa Msumbiji.

Aidha mafuriko hayo yamekuwa na athari ya moja kwa moja kwa watu 62,975 wa mikoa miwili ya Tete na Zambezia nchini Msumbiji.

 

Wakati huohuo, watu wanne wameripotiwa kuaga dunia kutokana na mafuriko hayo nchini Afrika Kusini.

 

Idadi ya wahanga wa majanga hayo ya kimaumbile yanatazamiwa kuongezeka kutokana na kimbunga kikali cha Idai.

 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload