Julius Caesar auawa kwenye bunge la Senati mjini Roma-44 KK

March 15, 2019

Gaius Julius Caesar   [ aliuawa tarehe 15 Machi 44 KK] alikuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi wa Roma ya Kale.

 

Anakumbukwa hasa kwa mafanikio mbalimbali yanayoonekana kuathiri dunia hadi leo;

Baadhi ya mafanikio hayo

 

1.Kama kiongozi wa kijeshi aliteka Gallia (leo: Ufaransa) na kuifanya jimbo la Kiroma. Kutokana na hiyo lugha ya Kifaransa ni karibu sana na Kilatini, lugha ya Roma ya Kale.

 

2.Waroma wa Kale walimheshimu kushinda viongozi wote waliomfuata au kutangulia akatangazwa kuwa mungu.

 

Jina lake lilipata kuwa neno kwa ajili ya cheo cha watawala wa Kiroma waliomfuata.

Kutokana na badiliko hilo la jina "Caesar" kuwa cheo, lugha mbalimbali zilipokea cheo hicho kama vile Kijerumani ("Kaiser"), Kirusi ("Tsar") na Kiswahili ("Kaisari" - kutokana na neno la Kijerumani ).

 

3.Aliunda kalenda ambayo imekuwa msingi wa kalenda ya kimataifa leo (Kalenda ya Juliasi). Kwa heshima yake, mwezi wa saba unaitwa Julai.

 

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon