Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Vijana wa Kipalestina waendelea kuuawa na askari katili wa Israel

March 13, 2019

Utawala katili wa Israel umeendelea kumwaga damu za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

 

Katika taarifa, Wizara ya Afya ya Palestina imesema vijana wawili wa Kipalestina waliuawa kikatili hapo jana, kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

 

Taarifa hiyo imesema mmoja wa mabarobaro hao wa Kipalestina waliouawa shahidi ni kijana wa miaka 23 kwa jina Mohammad Shaheen, ambaye alipigwa risasi kifuani baada ya kuvutana na wanajeshi wa Israel katika mji wa Salfit.

 

Jeshi la Israel liliuvamia mji huo mapema jana, katika operesheni ya kung'oa kamera za barabara za mji huo, jambo ambalo liliwaghadhabisha vijana wa Kipalaestina waliokuwa wakipinga uvamizi huo.

Wanajeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan

 

 kijana mwingine wa Kipalestina kwa jina Yasser Fawzi Shawki aliuawa  katika mji wa al-Khalil (Hebron) katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel, waliodai kuwa alitaka kuwashambulia kwa kisu.

 

Shirika la Hilali Nyekundu limesema liliwatibu Wapalestina 40 waliopata majeraha ya risasi na kuvuta gesi ya kutoa machozi waliovurumishiwa na askari wa Kizayuni katika uvamizi huo wa jana katika Ukingo wa Magharibi.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload