Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Amnesty International: Mahakama za Denmark hazichukui hatua kali kwa kesi za ubakaji

March 13, 2019

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekosoa vikali udhaifu wa vyombo vya usalama na mahakama vya Denmark katika kukabiliana na ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia na ubakaji nchini humo.

 

Amnesty International imeitaja Denmark kuwa ni moja ya nchi zenye utamaduni wa ongezeko kubwa la ukatili wa kijinsia na ina udhaifu mkubwa katika kukabiliana na kesi hizo.

 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia vinavyoripotiwa nchini humo, hupuuzwa au kufuatiliwa kwa udhaifu sana na jeshi la polisi suala ambalo limewafanya wahanga kushindwa kuripoti kwa jeshi hilo.

 

Imeongeza kwamba, hata wakati wanawake wanapowasilisha kesi hizo kwa polisi, jeshi hilo huonesha udhaifu mkubwa wa kumchukulia hatua au kumfunga muhusika wake.

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International

 

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limeongeza kwamba, takwimu za vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini Denmark ni za kutisha na jambo baya zaidi ni namna ambavyo kesi hizo zinafuatiliwa na vyombo vya mahakama.

 

kiasi kwamba, kati ya kesi 5000 zilizotokea mwaka 2017, ni wanawake 890 pekee walioweza kuwasilisha kesi zao mbele ya vyombo hivyo vya sheria na hatimaye kesi 94 pekee tu ndizo zilisajiliwa kwamba zimefuatiliwa kisheria.

 Ripoti hiyo imetolewa katika hali ambayo kwa mujibu wa takwimu za kimataifa, Denmark ni nchi inayojinadi kuchunga usawa wa kijinsia.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload