UN: Kimbunga na mafuriko yameua watu 10 Msumbiji


Takribani watu 10 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Msumbiji.

Ofisi ya Uratibu ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeripoti kuwa, watu sita wameaga dunia baada ya kusombwa na mafuriko hayo katika mkoa wa Tete ulioko katikati mwa nchi.

Aidha wengine wanne wamefariki dunia kutokana na janga hilo la kimaumbile katika mkoa wa pwani wa Zambezia.

Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na taasisi hiyo ya UN imesema kuwa, mvua, kimbunga cha Idai na mafuriko yamekuwa na athari ya moja kwa moja kwa watu 62,975 wa mikoa hiyo miwili.

Ramani ya Msumbiji

Kimbunga kikali cha kitropiki cha Idai kinachosafiri kilomita 100 kwa saa kinaripotiwa kuikumba nchi hiyo ya kusini mwa Afrika siku ya Jumamosi.

Watu 800 walipoteza maisha katika mafuriko mengine nchini Msumbiji mwaka 2000, huku wengine 100 wakiaga dunia kutokana na janga hilo mwaka 2015.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu