Shirika la Ndege la Boing, lafuta maonyesho ya ndege zake mpya kufuatia ajali ya ndege ya jana


Shirika la ndege la Boeing limesitisha maonyesho ya ndege zake mpya aina ya 777 X kufuatia kuanguka ndege ya shirika hilo ya Shirika la Ndege ya Ethiopia.

Shirika hilo limesitisha maonyesho ya ndege yake mpya yaliyokuwa yamepangwa kufanyikka siku ya Jumatano ya mwezi huu. Taarifa iliyotolewa na Shirika la Boeing imesema kuwa, maonyesho hayo hayatofanyika tena.

Hii ni katika hali ambayo Shirika la ndege la China nalo limesimamisha safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo, imesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa kufuatia ajali ya kudondoka ndege mbili aina ya Boeing 737 ikiwemo ya shirika la ndege la Indonesia na Ethiopia tangu miezi sita iliyopita. Kufuatia hali hiyo Shirika hilo limesimamisha safari za aina hiyo ya ndege.

Shirika la ndege la China ambalo nalo limefuta safari za ndege aina Boeing 737 nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uamuzi huo umekuja baada ya kubainika kwamba raia wanane wa China ni miongoni mwa karibu watu 150 waliopoteza maisha katika ajali ya ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia hapo jana.

Ndege hiyo ambayo sababu za kuanguka kwake bado haijabainika, ilikuwa inatokea mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia kuelekea jijini Nairobi Kenya.

Hayo yanajiri ambapo mwezi Oktoba mwaka jana pia ndege nyingine aina ya Boeing 737 ilianguka nchini Indonesia kwa sababu za hitilafu za mitambo dakika chache baada ya kuruka. Aidha ajali ya ndege ya Ethiopia nayo ilitokea muda mfupi baada ya kuruka.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu