Kumbukukumbu ya kuzaliwa ya mhandisi na mvumbuzi wa taa ya solar kutoka nchini Kenya


Evans Wadongo (amezaliwa 11 Machi 1986) ni mhandisi kutoka nchini Kenya, mwenyekiti wa chama kisicho cha serikali "Sustainable Development For All-Kenya (SDFA-Kenya)"

na mvumbuzi wa taa ya solar kwa ajili ya watu wanaoishi mashambani bila umeme.

Alipokuwa mwanafunzi alivumbua 2004 taa ya solar aliyoita "MwangaBora" akiwaza matumizi ya nishati ya jua kuwa njia njema ya kuhifadhi mazingira.

kupunguza kukatwa kwa miti na kuboresha maisha ya watu mashambani wanaoishi katika mazingira pasipo na umeme jinsi ilivyokuwa katika kijiji chake wakati alipokuwa mtoto mwenyewe.

Hakuvumbua taa za solar lakini alitumia teknolojia iliyokuwepo katika nchi zilizoendelea na kuilinganisha na mazingira ya Kenya.

Pamoja na wengine aliunda chama kisicho cha serikali Sustainable Development For All-Kenya (SDFA-Kenya) kilichoendelea kusambaza wazo la kutumia nishati ya jua kwa kuboresha maisha ya watu.

Taa ya solar inatengenezwa kwa bei nafuu na wafundi Wakenya kwa kutumia mabaki ya metali kutoka viwandani na karahana na diodi za LED zinazotumia umeme kidogo.

Mwaka 2010 shirika la habari la CNN ilitambua sifa zake kwa kumpatia cheo cha "Mshujaa wa CNN" katika ya chaguo la "top ten heroes of 2010". Mwaka 2011 alikabidhiwa tuzo la mfuko wa Mikhail Gorbachev kwa "watu waliobadilisha dunia"

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu