Zaidi ya magaidi 121 watiwa mbaroni nchini Pakistan


Askari jeshi wa Pakistan wamefanikiwa kuwatia mbaroni magaidi 121 katika operesheni maalumu ya jeshi hilo ya kupambana na magaidi katika kona mbalimbali za nchi hiyo.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo leo na kuongeza kuwa, askari wa Pakistan wameendesha operesheni kabambe ya kuwasaka magaidi kwa kupekua shule 182 za kidini katika maeneo tofauti ya nchi hiyo na kuwatia nguvuni magaidi 121. Hata hivyo hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusiana na habari hiyo.

Idara ya Kupambana na Ugaidi ya Pakistan (NACTA) hivi karibuni ilitangaza orodha ya magenge 68 yaliyopigwa marufuku nchini humo huku genge la kigaidi linalojiita Jundullah ambalo mara kwa mara linafanya vitendo vya kigaidi ndani ya ardhi ya Iran ni miongoni mwa magenge hayo ya kigaidi yaliyomo kwenye orodha hiyo ya jeshi la Pakistan.

Wanajeshi wa Pakistan

Genge hilo linatumia ardhi ya Pakistan kupanga mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wananchi wa Iran na mara kwa mara huvuka mpaka wa nchi hizo mbili na kufanya vitendo vya kigaidi ndani ya Iran.

Karibu miaka mitano iliyopita, Jeshi la Pakistan liliendesha operesheni ya "Pigo la Ghadhabu" dhidi ya magaidi na kuangamiza idadi kubwa ya magaidi hao katika maeneo tofauti ya Pakistan. Hivi sasa jeshi hilo limeanzisha operesheni nyingine liliyoipa jina la "Radul Fasad."

Magenge ya kigaidi kama vile Sipah-e-Sahaba, Daesh (ISIS) na Jamaat Ahrar Pakistan ni miongoni mwa magenge ya kigaidi yaliyomo kwenye orodha hiyo ya jeshi la Pakistan.

www.mzunuko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu