Trump atoa kauli baada ya Korea Kaskazini kukarabati eneo la kufanyia majaribio ya makombora


Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa, uamuzi wa Korea Kaskazini wa kukarabati eneo la kufanyia majaribio ya makombora, unazuia njia ya kuboresha uhusiano wa pande mbili.

Trump ameyasema hayo akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kwamba ripoti zilizotolewa kuhusiana na uamuzi wa serikali ya Korea Kaskazini wa kukarabati eneo la kufanyia majaribio ya makombora yake, ni zenye kuvunja moyo.

Jumanne iliyopita vyombo vya habari vilionyesha picha za satalaiti zilizoonyesha kuwa Pyongyang inalifanyia ukarabati eneo hilo lililo karibu na mpaka wa China.

Kabla ya hapo Korea Kaskazini na katika kuonyesha nia njema katika mazungumzo yake na Marekani iliamua kuliharibu eneo hilo la kufanyika majaribio ya silaha zake za nyuklia.

Kikao kilichovunjika mjini Hanoi, Vietnam na hivyo kutoa pigo kwa Trump.

Kikao cha duru ya pili kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na Kim Jong-Un wa Korea Kaskazini kilifanyika tarehe 27 na 28 za mwezi jana mjini Hanoi,Vietnam, kikao ambacho kilivunjika kabla ya kumalizika kwake.

Ujumbe wa Korea Kaskazini ulisema kwamba kupenda makubwa kwa Trump katika mazungumzo hayo, ndiyo sababu iliyopelekea kuvunjika kwake.

Katika kikao cha kwanza kati ya viongozi hao wa Marekani na Korea Kaskazini kilichofanyika nchini Singapore tarehe 12 Juni mwaka jana, pande mbili zilitiliana saini makubaliano ambayo yaliitaka Pyongyang kuangamiza silaha zake za nyuklia huku kwa upande wake Marekani nayo ikitakiwa kuidhaminia usalama nchi hiyo.

Hata hivyo Marekani haikutekeleza mapatano hayo suala ambalo daima limekuwa likilalamikiwa kila mara na Korea Kaskazini.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu