Mayahudi wanaoishi Marekani wamuunga mkono mbunge Mwislamu wa nchi hiyo 'Ilhan Omar'

March 6, 2019

Kundi la Mayahudi wanaoishi nchini Marekani wametangaza uungaji mkono wao kwa Ilhan Omar, mbunge Mwislamu wa nchi hiyo kutokana na misimamo yake ya ukosoaji siasa chafu za Washington kuhusu utawala haramu wa Israel.

 

Kundi hilo la Mayahudi wanaishi Marekani sambamba na kufika katika ofisi ya  Rashida Tlaib, mbunge mwingine wa bunge la Marekani mwenye asili ya Palestina, wametangaza kumuunga mkono Omar kutokana na ukosoaji wake kwa utawala wa Kizayuni na pia siasa mbovu za Marekani kwa utawala huo.

 

Ariel Gold, mwanaharakati wa amani na mwanachama wa kundi la Code Pink, sambamba na kusisitiza udharura wa kubadilishwa siasa za Marekani kuuhusu utawala huo wa Kizayuni, amesema:

 

"Kuna udharura wa kuwapeleka wananchi wa Marekani katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ili wajionee kwa macho yao wenyewe, kwani kuna hali ya kusikitisha sana."

Ilhan Omar, mbunge Mwislamu wa nchini Marekani

 

Mwanaharakati huyo na mtetezi wa haki za Wapalestina ameongeza kwamba, ni jambo muhimu kwa kadhia ya Wapalestina kuwasilishwa katika nchi zote duniani kama ambavyo pia ni muhimu kuwauliza wagombea urais wa Marekani katika uchaguzi wa 2020 kwamba ni kwa nini Washington ni lazima kuupatia utawala wa Kizayuni kiasi cha zaidi ya Dola bilioni tatu kila mwaka na hivyo kushiriki katika ukiukaji wa haki za binaadamu?

 

Hayo yanajiri katika hali ambayo baadhi ya wabunge wa Republican na hata wengine wa chama cha Ilhan Omar yaani chama cha Democrat, wameunda kambi ya upinzani dhidi ya mwanasiasa huyo Mwislamu kutokana na hatua yake ya kuukosoa utawala wa Kizayuni tangu alipochaguliwa katika bunge la nchi hiyo. Ilhan Omar ameitaja lobi za Kizayuni katika kuingilia siasa za Marekani kuwa haribifu.

 

Aidha amesema kuwa lobi hizo za Kizayuni zimekuwa zikitoa fedha kuwanunua wabunge wa Marekani kwa ajili ya kuutetea utawala haramu wa Israel katika bunge la nchi hiyo.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon