Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri nchini Tanzania yazidi kuzua maswali mengi

March 4, 2019

Hatua ya Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kufanyia mabadiliko madogo baraza lake la mawaziri imeendelea kuzua maswali mengi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

 

Wadadisi wa mambo wanasema, mawaziri aliowateua katika nyadhifa mpya walikuwa wachapa kazi katika wizara zao za awali. Itakumbukwa kuwa, katika mabadiliko hayo, Rais Magufuli alimteua Balozi. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

 

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mahiga alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Aidha Rais Magufuli alimteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huo Prof. Kabudi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

 Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo na mbunge wa Kigoma amendika katika mtandao wake wa Twitter kuwa, mabadiliko hayo ni hatua kubwa kwa Tanzania kuelekea kutiwa saini kwa mkataba wa kibiashara kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya na hali kadhalika kutolewa kwa nafasi ya mashauriano ya kisiasa.

Augustine Mahiga Waziri mpya wa Katiba na Sheria nchini Tanzania

 

Augustine Mahiga Waziri mpya wa Katiba na Sheria nchini Tanzania

Fumbuka Ng'wanakilala, mwandishi wa habari, Tanzania anasema Balozi Augustine Mahiga ni mwanadiplomasia aliyebobea, lakini anaonekana kama ni mtu mpole.

 

Kwa upande wake Prof Palamagamba Kabudi, ambaye amewahi kuwa mwalimu wa sheria chuo kikuu, anaonekana ni mtetezi mahiri wa sera za serikali ya Rais John Magufuli.

 

Mabadiliko haya madogo ya baraza la mawaziri yanakuja wakati uhusiano wa Tanzania na baadhi ya nchi za magharibi unaonekana kutetereka.

 

Baadhi ya mabalozi wa nchi za magharibi hivi karibuni wameanza kutoa matamko hadharani kuhoji demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania.

 

''Namuona Profesa Kabudi kama mtu anayeweza kuwakumbusha hadharani pia mabalozi wa nchi za magharibi kuzingatia Mkataba wa Vienna na kutoingilia masuala ya ndani ya Tanzania''. ailsema Fumbuka Ng'wanakilala.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon