Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Bouteflika: Nitaitisha uchaguzi wa mapema nikichaguliwa tena

March 4, 2019

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ameahidi kwamba hatahudumu kwa muhula kamili iwapo atachaguliwa tena kama rais katika uchaguzi wa mwezi Aprili, baada ya maandamano makubwa kufanyika nchini humo.

Maandamano hayo yalikuwa yanapinga harakati zake za kuongeza muda kwenye miaka ishirini aliyotawala. Kituo cha televisheni cha Ennahar kinasema kuwa ameahidi kuachia ngazi baada ya mwaka mmoja iwapo atachaguliwa.

 

Tangazo hilo lililosomwa kwa niaba yake na mkurugenzi wake wa kampeni Abdelghani Zaalane lilisema rais huyo amepanga kuandaa uchaguzi mpya mapema.

 

Mkurugenzi wa kampeni aliwasilisha nyaraka baada ya tangazo

 

"Uchaguzi mpya wa urais utafanyika tena ambao utatokana na mkutano wa kitaifa tutakaofanya. Naahidi sitagombea tena urais katika uchaguzi huo," alisema Abdelghane, "lengo la uchaguzi huo ni kuhakikisha makabidhiano ya madaraka kwa njia ya amani na mazingira yaliyo huru na wazi. Mkutano huo wa kitaifa ndio utakaoamua tarehe ya uchaguzi," aliongeza mkurugenzi huyo.

Waandamanaji wakiandamana dhidi ya hatua ya Bouteflika kuwania urais tena

 

Mara tu baada ya tangazo hilo kutolewa mkurugenzi huyo wa kampeni aliwasilisha nyaraka zake za kugombea kiti hicho katika uchaguzi wa Aprili 18 kuelekea muda wa mwisho wa kuwasilisha nyaraka hizo uliokuwa umewekwa  saa sita usiku wa jana Jumapili.

 

Kabla tangazo hilo mkuu wa tume ya uchaguzi Abdelwahab Derbal alisema wagombea woteni sharti wawasilishe nyaraka zao binafsi, kwa hiyo iwapo hilo litazingatiwa basi huenda Bouteflika asiruhusiwe kugombea.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload