Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaunga mkono ripoti ya UN kuhusu jinai za Israel


Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League, imeunga mkono ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinai ambazo zinatendwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.

Saeed Abu Ali, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema: "Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina imetayarishwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Jana wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliripoti kuwa, Israel imefanya jinai dhidi ya binadamu katika kukandamiza maandamano ya raia wa Ukanda wa Gaza.

Ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa imesema, ushahidi unaonesha kuwa utawala wa Israel ulifanya jinai dhidi ya binadamu wakati wa kukabiliana na maandamano ya amani ya mwaka 2018 ya Wapalestina katika eneo la Ukanda wa Gaza.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakiwalenga kwa risasi Wapalestina wanaoandamana kwa amani GhazaWanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakiwalenga kwa risasi Wapalestina wanaoandamana kwa amani Ghaza.

Ripoti hiyo imesema kuwa, walenga shabaha wa Israel walikuwa wakiwapiga risasi kwa makusudi watoto wadogo, wafanyakazi wa uokoaji na waandishi wa habari.

Kufuatia ripoti hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unapaswa kuwajibika mbele ya jamii ya kimataifa.

Tangu tarehe 30 Machi mwaka jana Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wamekuwa wakifanya maandamano yaliyopewa jina la Haki ya Kurejea katika kila siku za Ijumaa.

Tangu wakati huo jeshi la Israel limekuwa likishambulia maandamano hayo ya amani na hadi sasa limeua raia wasiopungua 260 wa Palestina na kujeruhi wengine wasiopungua elfu 27.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu