Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Rais Nicolás Maduro: Ni lazima Juan Guaidó atiwe mbaroni baada ya kurejea nchini Venezuela

February 28, 2019

Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amesema kuwa, iwapo Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani ambaye hadi sasa yuko nje ya nchi atarejea nyumbani, atatiwa mbaroni mara baada ya kuwasili nchini humo na kupandishwa kizimbani.

 

Maduro ameyasema hayo Jumatano ya jana na kuongeza kwamba, ni lazima Guaidó atiwe mbaroni iwapo tarejea Venezuela kutoka Colombia na kufunguliwa mashtaka kutokana na hatua yake ya kukiuka sheria za nchi hiyo.

 

Maduro ameyasema hayo akijibu swali juu ya uwezekano wa kukamatwa kiongozi huyo wa upinzani na kuongeza kwamba, ni mahakama pekee yenye uwezo wa kuchukua uamuzi huo. Ijumaa iliyopita,

 

Juan Guaidó ambaye alijitangaza kuwa rais mpya wa Venezuela alivuka mpaka wa Venezuela na kuingia Colombia katika hali ambayo awali serikali ya Caracas ilimzuia kuondoka nchini humo.

 

Juan Guaidó, Kiongozi wa upinzani wa Venezuela aliyejitangazia urais kinyume na sheria kutokana na uungaji mkono wa Marekani.

 

Mapema jana Juan Carlos Valdez, Naibu Jaji wa Jopo la Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Venezuela alitangaza kwamba kiongozi huyo wa upinzani aliyejitangaza kuwa rais wa mpito wa Venezuela anakabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela kutokana na hatua yake ya kukiuka agizo la kumtaka asitoke nje ya nchi, lililotolewa na Mahakama ya Juu nchini humo.

 

Kwa mujibu wa  Carlos Valdez, kiongozi huyo wa upinzani amejiweka katika hatari ya kufungwa miaka 30 jela iwapo atarejea nchini humo. 

 

Hii ni kusema kuwa, licha ya Juan Guaidó kujitangaza kuwa rais wa Venezuela na kuungwa mkono na Marekani na nchi za Magharibi, lakini hadi sasa hana nguvu yoyote kwa kuwa jeshi na vyombo vya mahakama vinamuunga mkono Rais Nicolás Maduro aliyechaguliwa kisheria.

 

Aidha zaidi ya nchi 60 za dunia zimeunda muungano wa kundi la waungaji mkono wa sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa na zimepinga uingiliaji wowote wa masuala ya ndani ya nchi nyingine ikiwemo Venezuela.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload