Wasiwasi wa Unicef kuhusu kuendelea kuuliwa watoto wa Yemen na utawala wa Aal Saud

February 26, 2019

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umeripoti kuwa kwa wastani watoto wa Kiyemeni wanane huuawa au kujeruhiwa kila siku kutokana na mashambulizi yanayotekelezwa na muungano vamizi unaoongozwa na Saudia huko Yemen.

 

 

Shirika la Unicef limetangaza kuwa mamilioni ya watoto wa Kiyemeni wanashuhudia machafuko na mapigano makali katika maeneo 31 yaliyokumbwa na hujuma za muungano huo vamizi ikiwemo miji ya al Hudaydah, Taiz, Hajjah na Sa'ada.

 

Saudi Arabia imetenda jinai chungu nzima dhidi ya matabaka mbalimbali ya wananchi wa Yemen katika vita ilivyoanzisha dhidi ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu, hata hivyo jinai za dhahiri na zisizo za dhahiri dhidi ya watoto wa Yemen zinaweza kutajwa kuwa jinai za kutisha zaidi kuwahi kutekelezwa na muungano huo vamizi unaoongozwa na Saudia nchini humo.

 Kuwaua au kuwajeruhi watoto wa Yemen si jinai pekee zinazofanywa na muungano huo vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya watoto wa Yemen.

 

Kuzingirwa pande zote Yemen na wakati huo huo kuzuia kutumwa misaada ya kibinadamu nchini humo kumekuwa na mtazamo  mbaya zaidi kuliko kitendo cha kuwaua na kuwajeruhi watoto wa Yemen; kwa sababu mipango hiyo iliyotumiwa na wavamizi hao imewasababishia njaa kwa makusudi watoto hao.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon