Rouhani: Iran itasaidia kuijenga upya Syria na kuirejeshea utulivu

February 26, 2019

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kushiriki katika utekelezaji wa mipango itakayoainishwa na serikali ya Syria katika kuijenga upya nchi hiyo ya Kiarabu.

 

Rais Rouhani aliyasema hayo katika mazungumzo yake na na Rais Bashar al Assad wa Syria hapa mjini Tehran  na kuongeza kuwa, serikali ya Iran kama ilivyokuwa huko nyuma, itaendelea kuisaidia na kushirikiana na Syria katika juhudi zake za kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo iliyoshuhudia vita na uharibifu mkubwa kwa miaka kadhaa sasa.

 

Rais wa Iran amebainisha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu iko tayari wakati wote kuimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi na Syria katika kiwango cha kiistratijia na kuongeza kuwa, Tehran iko tayari kuimarisha uhusiano wa pande mbili na Damascus katika nyuga mbalimbali.

 

Amesema ushirikiano wa pande kadhaa wa nchi za Mashariki ya Kati umechangia pakubwa katika kurejesha usalama na uthabiti katika eneo hili.

Rais wa Syria alipokutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon