Maelfu ya watoto wahajiri wanaozuiliwa nchini Marekani wanabakwa

February 26, 2019

Wizara ya Afya ya Marekani imepokea malalamiko zaidi ya 4,500 yanayohusu kudhalilishwa kingono watoto wahajiri wanaozuiliwa nchini humo.

 

Mbunge wa Kongresi ya Marekani, Ted Deutch, aliyafichua hayo jana Jumanne katika kikao cha Kamati ya Sheria ya Bunge la Wawakilishi, kilichokuwa kikijadili sera ya kikatili ya kuwatenganisha watoto wadogo na wazazi wao wahajiri katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico.

 

Amesema, "Ofisi ya Kuwapa Makazi Wakimbizi imepokea mafaili 4,556 ya watoto wadogo wahajiri ambao wamenajisiwa na kufanyiwa aina nyingine za unyanyasaji katika kambi za serikali wanakoishi, kati ya Oktoba mwaka 2014 na Julai mwaka 2018''

 

Kadhalika Wizara ya Sheria Marekani imepokea malalamiko zaidi ya 1,300 kutoka kwa wahajiri, zikiwemo tuhuma 178 za wao kubakwa na maafisa wa serikali katika kambi hizo.

Maandamano ya kupinga sera za kuwatenganisha wahajiri na watoto wao nchini Marekani

 

Hii ni katika hali ambayo, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa mwaka jana aliitaka serikali ya Marekani ikomeshe sera yake hiyo ya kikatili ya kuwatenganisha watoto wadogo na wazazi wao wahajiri katika mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Mexico.

 

Serikali ya rais wa nchi hiyo Donald Trump imewatenganisha maelfu ya watoto na wazazi wao ambao wametiwa nguvuni kwa tuhuma za kuingia katika ardhi ya Marekani kinyume cha sheria.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon