HRW: Polisi ya Kongo DR iliua watu 27 katika 'Operesheni ya Likofi'


Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliwaua watu 27 katika operesheni dhidi ya magenge ya uhalifu katika mji mkuu Kinshasa, mwaka jana

Ripoti iliyotolewa jana na shirika hilo imesema kuwa, baadhi ya watuhumiwa hao wa uhalifu waliuawa kwa kunyongwa na kisha miili yao kukatwa vipande vipande katika operesheni hiyo iliyopewa jina la 'Likofi

Human Rights Watch imesema ilifanya mahojiano na mashuhuda wapatao 80, familia za wahanga, maafisa usalama na watu wengineo wakati wakichunguza mauaji hayo.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limeikosoa vikali serikali ya DRC kwa kuwaua washukiwa wa uhalifu, badala ya kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Jenerali Sylvano Kasongo, Kamanda Mkuu wa Polisi mjini Kinshasa ambaye anatuhumiwa kuhusika katika operesheni hiyo kati ya mwezi Mei na Disemba mwaka jana amekadhibishwa na habari ya kufanyika operesheni hiyo. nakusema "Polisi Kinshasa haiui watu, bali inawakamata na kuwafikisha mbele ya sheria.''

Naye Vidiye Tshimanga, Msemaji wa Rais Felix Tshisekedi ambaye katika kiapo chake cha urais mwezi uliopita aliapa kupambana na ukiukaji wa haki za binadamu, amekataa kuzungumzia kadhia hiyo.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu