Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Trump: Mwanamke mwanachama wa DAESH (ISIS) hana ruhusa ya kuingia Marekani

February 21, 2019

 Rais Donald Trump wa Marekani amesema, Hoda Muthana, mwanamke ambaye ni mwanachama wa kundi la kigaidi la DAESH (ISIS), hana ruhusa ya kuingia nchini humo. Trump ametoa agizo hilo na kuashiria hatua zilizochukuliwa na serikali ya Washington katika kuanzisha na kuliunga mkono kundi hilo.

 

Kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa Twitter, rais wa Marekani amemwamuru waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo ahakikishe Hoda Muthana, mwanamke ambaye ni mwanachama wa Daesh haruhusiwi kurejea Marekani

 

Naye Pompeo ametangaza kupitia taarifa maalumu kwamba, Hoda Muthana si raia wa Marekani na hana sababu yoyote ya kisheria ya kufanya safari nchini humo

 

Miaka minne nyuma, mwanamke huyo aliondoka katika jimbo la Alabama nchini Marekani na kufanya safari ya kuelekea nchini Syria.

 

Na hii ni pamoja na kwamba, familia ya Hoda Muthana inasema, binti yao huyo amezaliwa Marekani, hivyo inapasa yeye na mwanawe wa miezi 18 waruhusiwe kurejea nchini humo

Hoda Muthana na mtoto wake

 

Kuwapokea waliokuwa wanachama wa kundi la kigaidi la DAESH, mbali na kuwa maudhui iliyozusha tofauti kubwa kati ya viongozi wa nchi za Ulaya, limegeuka pia kuwa tatizo kubwa kwa wanasiasa ndani ya nchi hizo.

 

Hivi karibuni, Trump aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter kuzitaka Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na nchi zingine waitifaki wa Marekani barani Ulaya ziwapokee watu hao vinginevyo akasisitiza kwa kusema: "Tutalazimika kuwatelekeza"

 

Na hii ni katika hali ambayo, nchi kama Uingereza na Uholanzi ni miongoni mwa wapinzani wakuu wa suala la kuwapokea wanachama wa zamani wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS).

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload