Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Syria: Tutarejesha udhibiti wa milima ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na Israel

February 21, 2019

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Faisal Mekdad amesema kuwa kukombolewa na kudhibitiwa upya milima ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni ni haki ya kisheria ya serikali na taifa la Syria.

 

Mekdad ameyasema hayo alipokutana na Marcelo Montaner, Mkuu wa Majeshi ya Uruguay aliyetembelea Syria akiwa pamoja na ujumbe wake na kuongeza kwamba, kwa mujibu wa azimio nambari 242 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na maazimio mengine ya umoja huo

 

miinuko ya Golan hadi kufikia  mwaka 1967, ni sehemu isiyokubali kutenganishwa na Syria

 

Amesisitiza kwamba kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa kitendo cha udhibiti wa utawala haramu wa Israel kwa milima hiyo ni kinyume na sheria na ni batili na kwamba serikali ya Damascus kwa kushirikiana na askari wa kulinda amani itakabiliana na uvamizi wowote wa utawala huo wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya Syria,sambamba na kuendelea kufichua na kudhibitia uungaji mkono wa Israel kwa makundi ya kigaidi na ukufurishaji.

 

Faisal Mekdad, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria

 

kwa upande wake  Marcelo Montaner, Mkuu wa Majeshi ya Uruguay amemueleza Faisal Mekdad, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria kwamba nchi yake itatuma kundi la askari kwa ajili ya kusimamia usitishaji vita nchini Syria.

 

Hii ni katika hali ambayo Jumatano usiku wakazi wa miinuko ya Golan na katika kumbukumbu za kutimia miaka 36 walifanya mgomo wa kupinga njama za utawala katili wa Kizayuni za kuiunganisha miinuko hiyo na Israel sambamba na kusisitiza kwamba historia na matukufu ya Golan ni mambo yasiyokubali kutenganishwa na Syria.

 

Miinuko hiyo ilikaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Kizayuni mwaka 1967 katika Vita vya Siku Sita vya utawala  wa uvamizi na nchi za Kiarabu.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload