Jeshi la Venezuela lachukua hatua kali za kuzima njama chafu za Marekani

February 21, 2019

Jeshi la Venezuela limechukua hatua madhubuti kwa ajili ya kuzima njama chafu za Marekani dhidi ya nchi hiyo

 

Katika uwanja huo, jeshi hilo limechukua hatua ya kuzuia kuingia meli katika bandari za nchi hiyo wakati huu kabla ya kuwasili shehena inayotajwa na Marekani kuwa ni ya misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya Venezuela.

 

Hii ni baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuendelea kuingilia mambo ndani ya Venezuela ambapo siku ya Jumatatu alidai kwamba, kitendo cha jeshi la nchi hiyo kuendelea kumuunga mkono Rais Nicolás Maduro kinahatarisha mustakbali na maisha yao.

 

Kutokana na hali hiyo Vladimir Padrino López, Waziri wa Ulinzi wa Venezuela amesisitiza kwamba, kutokana na kuongezeka vitisho vya Marekani, jeshi la nchi hiyo limeimarisha zaidi doria katika mipaka yote ya taifa hilo kwa ajili ya kuzima hatua yoyote ovu ya Washington.

 

Vladimir Padrino López, Waziri wa Ulinzi wa Venezuela

 

Kabla ya hapo pia Rais Nicolás Maduro sambamba na kumtaja Trump kuwa chanzo kikuu cha mgogoro wa Venezuela, alisema kuwa hataruhusu misaada ya Marekani kuingia nchi hiyo na kufafanua kuwa, kuruhusu misaada hiyo kutaifungulia milango Washington ya kuingilia zaidi masuala ya ndani ya nchi yake.

 Vilevile alifafanua kuwa, serikali ya Marekani inayopenda kujitanua inafanya kila iwezalo ili kuidhibiti Venezuela.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon