Marekani inaipa Saudia teknolojia ya silaha za nyuklia

February 20, 2019

Ripoti ya Bunge la Kongresi nchini Marekani imebaini kuwa utawala wa Donald Trump uko mbioni kuikabidhi Saudi Arabia teknolojia ya siri ya kuunda silaha za nyuklia

 

Ripoti ya Kongresi iliyotangazwa Jumanne imeonyesha kuwa, Rais Trump wa Marekani anahusika moja kwa moja katika jitihada za kuyawezesha mashirika ya Marekani ijenge vituo vya kuzalisha umeme wa nyuklia Saudi Arabia na kwamba teknolojia hiyo inaweza kutumika kuunda silaha za nyuklia

 

Taarifa zilizofichuka zinaonyesha mawasiliano baina ya wakuu wa utawala wa Trump na mashirika ya nishati ya nyuklia nchini humo kuhusiana na kadhia hiyo ya kuipa Saudia teknolojia ya nyuklia

Ripoti hiyo imebainisha kuwa, wataalamu wana wasiwasi kuwa teknolojia nyeti ya nyuklia ya Marekani ikiwa mikononi mwa Saudia inaweza kutumiwa na ufalme huo kuunda silaha za nyuklia na hivyo kuhatarisha usalama wa Mashariki ya Kati

Kongres imesema imeanzisha uchunguzi kuhusu hatua ya Trump kuiuzuia Saudia siri za kinyuklia za Marekani

 

Mrithi wa ufalme wa Saudia Mohammad bin Salman mwaka jana aliweka msingi wa kituo cha kwanza cha utafiti wa nyuklia nchini humo mwezi Novemba mwaka jana. Saudia imekataa kutia saini sheria za kuizuia kutumia teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya kijeshi.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon