Iran yatuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha katika ajali mgodini Zimbabwe


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametuma salama za rambirambi na kutoa mkono wa pole kwa serikali, wananchi na familia za wahanga wa ajali ya mgodini huko Zimbabwe.

Bahram Qassemi amebainisha kusikitishwa na ajali hiyo iliyotokea katika mgodi wa madini ya dhahabu karibu na mji wa Kadoma kusini magharibi mwa mji mkuu Harare.

Mgodi huo uliporomoka kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko. Hadi kufikia sasa makumi ya wachimba madini wameaga dunia

Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Tarehe 12 mwezi huu bwawa moja lililoko karibu na mji wa Kadoma umbali wa kilomita 140 kusini magharibi mwa Harare lilipasuka na kuporomoka na kusababisha kujaa maji katika mgodi huo.

Wachimba madini wasiopungua 60 wameaga dunia katika ajali hiyo. Kampuni inayomiliki moja ya migodi hiyo ya dhahabu ya Rio Zimbabwe imesema kuwa watu wamekuwa wakiingia migodini kinyume cha sheria kutafuta dhahabu. Dhahabu nyingi huchimbwa Zimbabwe kinyume cha sheria.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu