Malkia wa Pembe za ndovu afungwa miaka 17 Tanzania

February 19, 2019

'Ivory Queen': Mahakama Tanzania yamfunga 'malkia wa pembe za ndovu' Yang Feng Glan na wenzake miaka 17 jela

Malkia wa Pembe amefikishwa katika mahakama ya Kisutu leo

 

Raia wa China Yang Feng Glan anayefahamika kama 'Ivory queen' na washtakiwa wengine wawili wamehukumiwa miaka 17 jela baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo.

 

Bi Feng na wengine, Silvanus Matembo, na Philemon Julius Manase waliofikishwa hii leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wametiwa hatiani kwa mashtaka matatu, yanayohusu ulanguzi wa meno ya tembo ikiwemo uhujumu uchumi

 

Watatu hao walipandishwa kizimbani kujibu mashtaka yahusianayo na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya takriban dola milioni 6

Ulanguzi wa Pembe za tembo umechangia kuongezeka kwa visa vya uwindaji haramu

 

Kifungo hicho kinaweza kupungua mpaka kwa miaka miwili iwapo watalipa faini ya thamani ya mara mbili ya nyara walizovuna.

 

Mahakama imeeleza kwamba ushahidi umetolewa na watu 11 wakiwemo wasafirishaji.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon