Saudia na Imarati zataka kuzusha ghasia katika mipaka ya Iran

February 18, 2019

Mashirika ya ujasusi ya Saudi Arabia na Umoja wa Falame za Kiarabu, Imarati, yameandaa mipango ya kuzua ghasia na machafuko katika mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

 

Hayo yalidokezwa Jumamosi na Brigedia Generali Muhammad Ali Ja'ffari, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, aliposhiriki mazishi ya mashihidi wa shambulio la kigaidi la hivi karibuni huko katika mkoa wa Sistan Baluchestan yaliyofanyika mjini Isfahan.

 

Amesema: Tuna ushihidi wa kutosha kwamba mashirika ya kijasusi ya Saudia na Imarati, yanafanya njama kubwa za kuchochea ghasia na ukosefu wa usalama,  hasa katika maeneo ya kusini mashariki mwa nchi, kwa kutilia maanani mazingira maalumu yanayotawala katika maeneo hayo ya Baluchestan ya Iran na Pakistan.

 

Jumatano tarehe 13 Februari, basi lililokuwa limewabeba askari walinzi wa mipaka wa Iran lilishambuliwa na magaidi katika njia ya Khash-Zahedan, katika mkoa wa Sistan na Baluchestan, kusini mashariki mwa Iran ambapo askari 27 waliuawa shahidi na wengine 13 kujeruhiwa.

Brigedia Generali Muhammad Ali Ja'ffari, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

 

Kundi la kigaidi la Jeshi la Dhulma lilitangaza kuhusika na shambulio hilo, likiwa na lengo la kuonyesha kuwa Jamhuri ya Kiislamu haina uwezo wa kudhamini usalama katika mipaka yake

Mazishi ya mashahidi waliouawa na magaidi Zahedan

 

Njama za Saudia za kutumia magaidi katika kuzua ghasia na machafuko nchini Iran zilidhihirika wazi kufuatia hatua ya Turki bin Faisal, mwanasiasa na mmoja wa watu mashuhuri katika ukoo wa Saud kushiriki katika kikao cha kila mwaka cha kundi la kigaidi la Munafiqeen huko mjini Paris.

Turki bin Faisal akishiriki mkutano wa kila mwaka wa magaidi wa Munafiqeen mjini Paris, Ufaransa.

 

Watawala wa Saudia wamekuwa wakichukua hatua mbovu na za makosa katika uwanja huo na baadhi ya nchi kama vile Pakistan zimekuwa wahanga wa siasa hizo za watawala wa Saudia ambapo kudumishwa kwa siasa hizo bila shaka kutazidhuru nchi hizo zenyewe.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon