Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Israel inazifanyia majaribio silaha zake kwa watoto wa Kipalestina

February 18, 2019

 Profesa mmoja anayehadhiri katika Chuo Kikuu cha Hebrew kilichoko katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) amesema, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel linazifanyia majaribio silaha zake mbalimbali kwa Wapalestina, wakiwemo hata watoto wadogo ili kuweza kuelewa ni zipi zenye nguvu na uwezo mkubwa zaidi.

 

Profesa Nadera Shalhoub-Kevorkian ameyasema hayo katika mhadhara aliotoa kwenye Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani na kuongeza kuwa, Israel inafanyia majaribio silaha zake kwa watoto wa Kipalestina na kwamba maeneo ya Palestina ni maabara kwa ajili ya sekta ya usalama ya Israel.

 

Katika mhadhara wake huo aliotoa kwa anuani ya "Teknolojia za Ukatili katika Jerusalem ya Palestina", Profesa huyo wa kazi za kijamii katika Chuo Kikuu cha Hebrew amenukuu ushahidi wa maelezo yaliyotolewa na watoto kadhaa kuthibitisha kuwa jeshi la Israel linakilenga zaidi kizazi cha vijana hao wadogo kwa ajili ya kuzifanyia majaribio silaha zake.

Profesa Nadera Shalhoub-Kevorkian

 

Chuo Kikuu cha Hebrew hakijatoa kauli yoyote ya kupinga au kulaaani maelezo hayo zaidi ya kusema, maoni yaliyotolewa na Profesa Nadera Shalhoub-Kevorkian hayaakisi mtazamo wa chuo hicho.

 

Shutuma hizo mpya dhidi ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel zimetolewa katika hali ambayo, kabla ya hapo, vyombo kadhaa vya habari viliripoti kuwa, jeshi hilo la utawala huo ghasibu linanyofoa viungo vya watoto wadogo wa Kipalestina linaowaua.

 

Mnamo mwezi Novemba mwaka 2015, Riyadh Mansour, balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa aliwahi kumwandikia barua Katibu Mkuu wa umoja huo kumweleza kwamba,

 

maiti za Wapalestina waliouliwa na askari wa Israel na kurejeshwa kwa jamaa zao zimegundulika kuwa hazina kornea na viungo vyengine, hali inayothibitisha ukweli wa ripoti kuhusu unyofoaji viungo unaofanywa na utawala huo haramu.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload