Askari tisa wa Saudi Arabia waangamizwa kusini mwa nchi hiyo


Jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi vimesambaratisha operesheni tatu mtawalia zilizofanywa na askari wa vikosi vamizi vya Saudi Arabia kwa lengo la kusonga mbele kuelekea ngome zao magharibi mwa eneo la Majazah mkoani Asir kusini mwa nchi hiyo.

Katika mapigano hayo yaliyotokea jana, jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi, vilifanikiwa kuwaangamiza askari tisa wa Saudia na kuwajeruhi makumi ya wengine.

Wakati huohuo kikosi cha mizinga cha jeshi la Yemen likishirikiana na wapiganaji wa kujitolea kimevishambulia kwa makombora vituo vya mikusanyiko ya mamluki wa Saudi Arabia kando kando ya kivuko cha A'lab na eneo la al-Rabu'a katika mkoa huo huo wa Asir

Licha ya Yemen kuwekewa mzingiro wa pande zote na utawala wa Aal Saud, uwezo na nguvu za kujihami za jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa nchi hiyo zinazidi kuongezeka siku baada ya siku.

Wapiganaji wa harakati ya Ansarullah ya Yemen

Mnamo mwezi Machi 2015, kwa uungaji mkono wa Marekani, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na baadhi ya nchi nyingine, Saudi Arabia ilianzisha uvamizi na mashambulio ya kijeshi dhidi ya Yemen, sambamba na kuiwekea mzingiro wa nchi kavu, angani na baharini.

Uvamizi wa kijeshi wa Saudia na waitifaki wake umesababisha maafa makubwa ya roho za watu pamoja na uhaba mkubwa wa chakula na dawa nchini Yemen.

Hata hivyo, baada ya karibu miaka minne ya mauaji ya maelfu ya raia wasio na hatia, mbali na kuwajeruhi maelfu na kuwafanya wakimbizi mamilioni ya wengine sambamba na kubomoa miundomsingi ya Yemen,

mugawano wa wananchi wa Yemen, umeufanya utawala wa Aal Saud na waitifaki wake washindwe kufikia malengo yao ya kuisambaratisha harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah na kumrejesha madarakani kibaraka wao Abd Rabbu Mansou Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutorokea huko Saudia

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu