Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

BBC yakiri kuwa shambulio la silaha za kemikali Douma, Syria lilikuwa bandia

February 15, 2019

Picha za uongo zilizoenezwa na vyombo vya habari vya Magharibi kuhusu shambulio la kemikali nchini Syria.

 

Mwandishi wa habari wa shirika la utangazaji la BBC la utawala wa kifalme wa Uingereza amekiri kuwa shambulio la kemikali lililodaiwa kufanywa katika mji wa Douma nchini Syria mwaka 2018 lilikuwa bandia na hata London ilikuwa inatambua vyema kwamba hakuna gesi yoyote ya sumu iliyotumika kwenye mji huo.

 

Riam Dalati ametuma ujumbe kadhaa wa maandishi akisisitiza kuwa amefanya uchunguzi mwingi kuhusu madai ya kufanyika shambulio la silaha za kemikali tarehe 7 Aprili 2018 katika mji wa Douma wa Gouta Mashariki nchini Syria lakini amegundua kuwa madai yote yaliyotolewa kuhusu shambulio hilo au kutumika gesi ya kemikali ya sarin; ni uongo mtupu na hakuna ushahidi wowote wa kufanyika shambulizi kama hilo.

Magaidi wafanya jinai walioivamia Syria kila upande kwa msaada wa madola ya Magharibi na vibaraka wao.

 

Itakumbukuwa kuwa magenge ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu huko Syria mwezi Aprili 2018 zilishirikiana na vyombo vya habari vya maadui kama vile BBC kueneza picha za uongo na kudai kuwa eti serikali ya Syria ilifanya shambulio la kemikali katika mji wa Douma wakati huo.

 

Katika moja ya ujumbe wake wa karibuni kabisa alioutuma kwenye ukurasa wake wa Twitter, Dalati amefichua kwamba vyombo hivyo vya habari vilibuni habari hiyo ya uongo ili kuchochea fikra za walimwengu na kwamba serikali ya Uingereza ilikuwa na taarifa kuhusu uongo wa madai hayo.

 

Itakumbukwa kuwa kitendo hicho kiovu cha vyombo vya habari vya maadui kilitumiwa vibaya haraka sana na Marekani na Ufaransa kulishambulia jeshi la serikali ya Syria tarehe 14 Aprili 2018 hata kabla ya kufanyika uchunguzi kuhusu madai hayo na bila ya idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload