Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mlipuko wa bomu ya nyuklia ya kwanza unatokea nchini Ufaransa-1960

February 13, 2019

Mlipuko wa bomu la nyuklia la jaribio

 

Tarehe 13 februari mwaka 1960 kunatokea mlipuko wa  bomu ya nyuklia ya kwanza nchini Ufaransa.

Bomu la nyuklia ni silaha inayosababisha mlipuko mkubwa sana. Kati ya silaha zote, hiyo ni yenye nguvu na pia yenye hatari zaidi.

 

Nishati ya mlipuko huo inaweza kutokea kwa njia mbili

  • mwatuko nyuklia (kupasuliwa kwa kiini cha atomu kuwa elementi mbili)

  • myeyungano nyuklia (kuungana kwa viini viwili vya atomu kuwa elementi nzito zaidi).

Katika mmeyeyungano nyuklia sehemu ya mada ya atomu hugeuzwa kuwa nishati.

 

Mabomu ya kawaida hutumia nishati ya mmenyuko wa kikemia ambamo viini atomia havibadiliki.

Nishati inayopatikana kwa njia ya mmenyuko mfululizo wa kinyuklia ni kubwa sana. Bomu moja la nyuklia latosha kuharibu kabisa mji  kwa mfano  ilivyotokea mnamo Agosti1945 huko Hiroshima na Nagasaki. Mabomu hayo yalikuwa madogo sana kuliko mabomu yaliyotengenezwa baadaye.

 Tangu Nagasaki hakuna bomu lingine lililotumiwa vitani. Milipuko yote iliyofuata ilikuwa ya jaribio tu, ama jangwani au baharini pasipo watu. Nchi zote ziliogopa uharibifu mkubwa kupita kiasi, ingawa hasa nchi kubwa za Marekani na Urusi ziliendelea kutengeneza maelfu ya mabomu.

 

Tangu miaka ya 1980 imejulikana ya kwamba milipuko ya robo hadi nusu ya silaha za nyuklia zilizokuwepo tayari ingetosha kukomesha uhai duniani kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo ingetokea kwa sababu ya kiasi kikubwa cha vumbi kinachorushwa hewani na milipuko hii.

 

Vumbi hilo lingejaza anga na kuzuia nuru ya jua kufika kwenye uso wa dunia, hivyo kusababisha giza pamoja na kushuka kwa halijoto kwa muda wa miaka kadhaa.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload