Jeshi la Kongo DR laua magaidi wanne mjini Beni

February 13, 2019

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza habari ya kuangamiza wanachama wanne wa kundi la kigaidi la ADF, mashariki mwa nchi.

 

Kapteni Mak Hazukay, msemaji wa jeshi la Kongo DR katika mkoa wa Kivu Kaskazini amesema operesheni ya kuwaangamiza wanamgambo hao wa ADF ilifanyika jana Jumanne, katika eneo la Mamove, yapata kilomita 50 magharibi mwa mji wa Beni.

 

Amesema askari wa DRC wamefanikiwa pia kuwakomboa watu wanne waliokuwa wameshikwa mateka na magaidi hao.

 

Mwezi Disemba mwaka uliopita, watu wasiopungua 27 waliuawa katika mashambulizi mawili tofauti yaliyofanywa na kundi hilo la wanamgambo wa ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wanamgambo wa ADF

 

Magaidi hao wanaripotiwa kuua watu wasiopungua 58 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

 

Wanamgambo wa ADF wanaotokea Uganda walianzisha harakati zao mashariki mwa Kongo tangu mwaka 1994 na katika miaka hiyo yote wameuwa mamia ya raia wa eneo hilo, mbali na kuteka nyara makumi ya wengine haswa watoto.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon