Deni la taifa la Marekani lavunja rekodi, ni zaidi ya dola trilioni 22

February 13, 2019

Wizara ya Fedha ya Marekani imeripoti kuwa, nchi hiyo inadaiwa dola trilioni 22, kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.

 

Taarifa iliyochapishwa jana Jumanne na wizara hiyo inasema kuwa, deni hilo linatazamiwa kuongezeka kwa kiwango cha dola trilioni moja kwa mwaka, katika kipindi cha miaka kumi ijayo

 

Inaarifiwa kuwa, nakisi ya bajeti ya serikali imeongezeka hadi dola trilioni 2.06 tangu Rais Donald Trump aingie madarakani Januari mwaka 2017

 

Judd Gregg na Edward Rendell ambao ni wakuu wa vuguvugu la 'Fix the Debt' nchini Marekani wamesema kiwango hicho cha deni la taifa nchini humo kupindukia dola trilioni 22 ni kumbukizi nyingine chungu ya kuonesha kule inakoelekea nchi, na  athari  zake kwa vizazi vijavyo.

Marekani ndiyo nchi inayotajwa kuwa na uchumi mkubwa zaidi duniani

 

Oktoba mwaka jana, Wizara ya Hazina ya Marekani ilisema kuwa, nchi inayoidai fedha nyingi zaidi Marekani ni China. Kwa mujibu wa mtandao wa The Balance ni kuwa, hadi mwezi Julai mwaka jana wa 2018, China ilikuwa inaidai Marekani dola trilioni 1.17. 

 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Japan inaidai Marekani dola trilioni 1.05 ikifuatiwa na Brazil na Ireland ambazo zinaidai Marekani dola bilioni 300 kila moja. Uingereza inaidai Marekani dola bilioni 272.

 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon