Mashambulizi ya Kimtandao: Urusi yajipanga 'kuzima intaneti ili kujilinda na maadui'

February 12, 2019

Urusi inajipanga kuzima mtandao wa intaneti kwa muda, na hivyo kujitoa kwenye mawasiliano na dunia kama sehemu ya majaribio yake ya kujikinga dhidi ya mashambulio ya kimtandao.

Zoezi hilo litafanya mawasiliano baina ya raia na mashirika ya Urusi kubaki ndani ya nchi badala ya  kupitia njia za kawaida za kimtandao kimataifa.

 

Rasimu ya sheria ya kuruhusu mabadiliko ya kiufundi ili kuiwezesha nchi hiyo kuendesha mtandao wake wenyewe iliwasilishwa bungeni mwaka jana.

 

Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe mosi Aprili, lakini siku rasmi ya kuzimwa mtandao haijatajwa.

Rasimu hiyo ya sheria, iliyopewa jina la Programu ya Taifa ya Uchumi wa Kidijiti, inawataka watoa huduma za intaneti nchini Urusi kuwa na uwezo wa kuendelea na huduma zao hata pale ikitokea nchi za kigeni zikiamua kuitenga Urusi.

Nchi wanachama wa Nato na washirika wake wamekuwa wakitishia kuiwekea vikwazo vya kimtandao Urusi ambayo wanaituhumu kwa kufanya mashambulio ya kimtandao.

 Njia mojawapo inayopangwa na Urusi katika kujilinda huko ni kutengeneza mfumo wake binafsi wa anuani za kimtandao ufahamikao kama DNS, waweze kupata mawasiliano hata pale watakapotengwa ama kujitenga.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon