Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

ISIL bado ni tishio, juhudi za pamoja zahitajika kulisambaratisha- Voronkov

February 12, 2019

Uharibifu mkubwa uliofanyika Iraq mji wa Mosul ambako watu walipoteza maisha mikononi mwa kundi hilo.

 

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na ugaidi, Vladmir Voronkov amesema kuwa  mtandao wa magaidi wa ISIL unaendelea kuendesha operesheni zake kisiri huko mashinani nchini Syria na Iraq na kutishia harakati za kuleta utulivu nchini humo.

Vladmir Voronkov

 

Akiwasilisha ripoti ya 8 ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mbele ya Baraza la Usalama la umoja huo hii leo jijini New York, Marekani kuhusu tishio la ISIL  kwenye amani na usalama duniani, Bwana Voronkov amesema magaidihao wanaendelea kujiimarisha  hususan Iraq na Syria ambako yaripotiwa wanamiliki wapiganaji kati ya 14,000 hadi 18,000 wakiwemo 3,000 ambao ni wapiganaji wa kigeni.

 

Licha ya kuwa na operesheni za kisiri, utawala wa ISIL umeendelea kuwa na ushawishi na kuendeleza nia yake ya kufanya mashambulio kimataifa na hivyo kuendeleza malengo yao ya ugaidi,” amesema Voronkov.

Myazidi kutoka Sinjar nchini Iraq ambaye alitekwa nyara na kikundi cha ISIL, hapa yuko kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mamilyan huko Akre, nchini Iraq.

 

Kuhusu uwezo wa kifedha wa ISIL, Bwana Voronkov amesema licha ya kupoteza mapato yao kutokana na kudhibitiwa kwenye baadhi ya maeneo, bado kundi hilo linaweza kusongesha operesheni zake kwa kutumia akiba ya fedha ambayo ni kati ya dola milioni 50 hadi milioni 300.

 

 

“Vikundi vya ISIL vyaripotiwa kupata mapato kutokana na shughuli za kihalifu,” amesema Bwana Voronkov akienda mbali zaidi kutaja jinsi ambavyo kundi hilo linatandaza operesheni zake maeneo mbalimbali duniani.

 

Mathalani eneo la Kusini-mashariki mwa Asia, ripoti imebaini ongezeko la vijana na wanawake wanaojiunga na operesheni za ISIL lijulikanalo pia kama Da’esh kwenye ukanda huo akisema ni changamoto ambazo wanatumia mfumo wa kukabili changamoto hizo.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload