West Ham kuchunguzi matusi ya ubaguzi dhidi ya mshambuliaji wa Liverpool Salah


Timu ya West Ham inachunguza tukio la baada ya video iliyo sambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha shabiki mmoja akimshambulia, mshambuliaji wa timu ya Liverpool Mohamed Salah wakati wa mchezo uliochezwa mwanzoni mwa wiki , mchezo uliozaa sare ya bao moja moja kwenye uwanja wa London uliopigwa mwanzoni mwa wiki hii.

Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Misri Salah, mwenye umri wa miaka 26, alirekodiwa kwenye kipande cha video kwa njia ya simu upande walikokuwa wamekaa washabiki wa timu yake katika uwanja wa nyumbani wakati alipokuwa akijiandaa kuupiga mpira wa kona.

Kipnde hicho cha video, kilirekodiwa na shabiki wake, ikinaonesha akitupiwa maneno makali ikiwemo yake ya kiislam.

Katika taarifa yake, timu hiyo ya West Ham imearifu kuwa wao kama timu "wana sera ya kuvumiliana kwa kiwango kikubwa kwa aina yoyote ya tabia ya vurugu au ya mateso".na kuendelea kueleza kuwa Sisi ni klabu ya soka inayojumuisha.

Mtu yeyote anayejulikana kufanya kosa atatakiwa kutoa maelezo kwa polisi na atakabiliwa na marufuku maisha ya kutoingia kushuhudia mtanange wa timu hiyo na timu zingine katika viwanja hivyo vya London, hakuna nafasi ya tabia kama hizo katika viwanja vyetu.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu