Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Trump anaashiria ushindi wa mapambano dhidi ya IS

February 7, 2019

Rais Donald Trump anaashiria wafuasi wa itikadi kali wa Dola la Kiislam-IS watapokonywa ardhi yote wanayoidhibiti nchini Iraq na Syria. Matamshi hayo ameyatoa katika mkutano ulioitishwa katika wizara ya mambo ya nje.

Rais Donald Trump amewaambia wawakilishi wa muungano wa mataifa 79 yanayoongozwa na Marekani katika mapambano dhidi ya  wafuasi wa itikadi kali wa Dola la Kiislam au Daesh kwamba wanamgambo hao wanadhibiti sehemu ndogo tu ya ardhi wanayodai kuwa ni ya utawala wao au Khalifa.

 

"Wanajeshi wa Marekani, washirika wetu na vikosi vya kidemokrasi nchini Syria wameikomboa takriban ardhi yote iliyokuwa hapo awali ikidhibitiwa na IS nchini Syria na Iraq. Kimsingi habari hizo huenda zikatangazwa wakati wowote kutoka sasa, pengine wiki inayokuja, kwamba tunadhibiti asili mia kwa mia ya ardhi  au Khalifat. Lakini nataka kusubiri hadi tamko rasmi . Sitaki kulisema kabla."

 

Maafisa wa Marekani walisema IS wamepoteza asili mia 99.5 ya ardhi yao na kwamba wanadhibiti chini ya kilomita za mraba 5 nchini Syria, katika vijiji vya bonde la mto Euphrates.

Kambi zinazowahifadhi wasyria wanaokimbia mapigano ya IS

 

Hata hivyo kuna hofu, uamuzi wa kuondolewa wanajeshi wa Marekani usije ukavuruga matumaini hayo. Rais Trump amewaambia washirika katika mapambano dhidi ya IS waliokutana katika wizara ya mambo ya nchi za nje kwamba ingawa

 

"idadi ndogo ya waliosalia kutoka kundi hilo bado ni hatari" hata hivyo ameamua kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa Marekani. Amewatolea wito washirika wasimame kidete na kuchangia ipasavyo katika mapambano dhidi ya IS.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload