Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 07.02.2019: Hazard, Coutinho, Asensio, Maddison, Varane

February 7, 2019

James Maddison

 

Tottenham wana hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo wa kati wa Leicester na timu ya England James Maddison, kama mchezaji anayeweza kuichukua nafasi ya Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 26, iwapo mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Denmark ataondoka katika msimu wa joto.

Raphael Varane

Huenda Manchester United ikamlenga mlinzi wa Real Madrid Raphael Varane, mwenye umri wa miaka 25, kama mchezaji mkuu wanayemwinda katika dirisha la msimu wa joto.

Eden Hazard

Chelsea itaitisha zaidi ya £100m kutoka kwa Real Madrid kumuuza Eden Hazard iwapo klabu hiyo ya Uhispania itawasilisha ombi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 - msimu huu wa joto.

Philippe Coutinho

 

The Blues inakagua hali ya mchezaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 26, kama mchezaji anayeweza kuichukua nafasi ya Hazard.

 

Real Madrid bado ina matumaini ya kumsajili Hazard kwa chini ya £100m na huenda ikamtumia Isco, mwenye miaka 26, au Marco Asensio, mwenye miaka 23, kama sehemu ya makubaliano hayo.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload