Hotuba ya rais Marekani: Trump atangaza mkutano mwingine na rais Kim Jong-un wa Korea kaskazini


Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza katika hotuba yake kwamba ataanda mkutano wa pili kujadili masuala ya nyuklia na kiongozi wa Korea Kaskazini mwezi huu.

katika hotuba yake iliyoambatana na kauli mbiu"Choosing Greatness", aliapa kwa mara nyingine kujenga ukuta mpakani.

Huku akihimiza umoja, kiongozi huyo wa Republican pia amesema jitihada za 'uchunguzi ulio na upendeleo' wa Democratic huenda ukaathiri ustawi wa Marekani.

Kwa ukali, wanachama wa Democrat wamemshutumu Trump kwa kupuuza maadili ya Marekani.

Hotuba hiyo kuu ya rais Trump imejiri baada ya pengo la muda mrefu kuwahi kushuhudiwa katika historia, la kusitishwa ufadhili kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.

Alichochea kufungwa kwa mashirika ya serikali kwa kuitisha ufadhili wa ukuta wa mpakani kati ya Marekani na Mexico na kuishia kubadili kauli hiyo baada ya wanachama wa Democrat kukataa wazi.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu