Chukua hatua sasa kutokomeza FGM ifikapo 2030-UN


Wakati wa kuchukua hatua ili kutokomeza ukeketaji au FGM, ifikapo mwaka 2030 ni sasa .

Wito huo wa pamoja umetolewa leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la idadi ya watu UNFPA, Dkt. Natalia Kanem, lakuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore na la linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women.Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Ngariba na mjukuu wake wa miaka 10 ambaye alikuwa anatarajiwa kukeketwa lakini anaumwa kwa hiyo bibi yake anasubiri naye ili aweze kumkeketa.

'Wakitolea mfano wa athari za mila hiyo potofu watu hao wamesema "Mary Oloiparuni alikuwa na umri wa miaka 13 tu alipolazimika kupitia kisu cha ngariba kwa uchungu mkali na kutokwa na damu kupita kiasi na uchungu umeendelea hadi leo.

miaka 19 baadaye ambapo kila alipojifungua watoto wake watano maumivu yake hayasemeki.”

Katika maadhimisho ya leo viongozi hao wamesisitiza dhamira yao ya kukomesha ukiukwaji huo mkubwa wa haki za binadamu ili mamilioni ya wasichana ambao bado wako hatarini kukeketwa ifikapo 2030 kutopitia machungu aliyopitia Mary.

Wameongeza kuwa kwa kuwa FGM ni aina mojawapo ya ukatili hauwezi kushughulikiwa bila kujumisha mifumo mingine ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kama ndoa za utotoni. Wakihimiza kwamba ili kukomesha FGM ni lazima kushughulikia mizizi ya kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia na kuuhakikisha uwezeshaji wa wanawake kijamii na kiuchumi.

Mwaka 2015 viongozi wa dunia kwa pamoja waliunga mkono utokomezaji wa FGM ifikapo mwaka 2030 kupitia ajenda ya maendeleo endelevu SDGs. Umoja wa Mataifa unasema hili ni lengo linalowezekana n ani lazima tuchukue hatua sasa kugeuza utashi wa kisiasa kuwa hatua. Viongozi hao wa Umoja wa Mataifa wakizitaja hatua hizo wamesema

“Katika ngazi ya taifa tunahitaji será mpya na sheria za kulinda haki za wasichana na wanawake ili waishi huru bila ukatili na ubaguzi na kwa nchi ambazo FGM bado inaendelkea kuwe na mipango ya serikali kukomesha vitendo hivyo na mipango ijumuishe bajeti kwa ajili ya elimu, afya ya uzazi, huduma za jamii na msaada wa

kisheria.”

"Katika ngazi ya kikanda, tunahitaji taasisi na jamii kufanya kazi pamoja kuzuia kitendo cha wanwake na wasichana kuvuka mipaka kwa lengo la kuwapeleka kwenye maeneo ambayo sheria kuhusu ukeketaji si kali sana ili wakafanyiwe ukatili huo.”

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu