Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Riwaya za kwanza za fasihi ya Japani-Hekaya ya Genji

February 6, 2019

Hekaya ya Genji  ni kati ya riwaya za kwanza za fasihi ya Japani.

 

Hadithi hii ya mwanamfalme Genji inasomwa na kuheshimiwa hadi leo katika utamaduni wa Japani.

 

Iliandikwa na mwandishi wa kike Murasaki Shikibu mnamo mwanzo wa karne ya 11 BK.

 Hadithi

 

Genji ni mwana wa mfalme Kiritsubo wa Japani na hawara (mke wa kando) anayependwa na baba yake lakini mfalme hawezi kumpa nafasi juu ya mrithi wake rasmi.

 

Kufuatana na mila anapewa jina tofauti ya familia Minamoto (aka Genji), hahitaji kufanya kazi, lakini anapewa mafunzo katika usanii na michezo ya kijeshi.

 

Akiwa na umri mdogo anaanza kutamani wanawake na ilhali ana cheo cha juu anaanza kutimiza tamaa zake. Anaanza mapenzi na wanawake wengi wa aina mbalimbali.

 

Baada ya kujiuzulu kwa mfalme  baba yake,  Genji anaondoka kwa hiari yake katika ikulu ya kifalme.

 

Wakati wa kukaa nje anamzaa mtoto wake wa kwanza lakini hawezi kurudi kwenye ikulu pamoja na mpenzi wake Murasaki.

 Anaendelea kufanya mapenzi na wanawake wengi, anashindwa kuwa mwaminifu kwa mmoja, akikaa na wanawake mbalimbali katika nyumba yake.

 

Baada ya kifo cha mpenzi wake, Genji hana nguvu ya kuishi tena. Riwaya haielezi jinsi gani anavyoaga dunia.

 

Sehemu ya mwisho ya riwaya inasimulia habari za wanawe Niou und Kaoru lakini pia hadithi hii inakwisha kwa ghafla.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload