Papa Francis amekiri kuwa makasisi wa kanisa katoliki wanawatumia watawa kama watumwa wa ngono

February 6, 2019

Papa Francis amekiri kuwa makasisi wa kanisa katoliki wanawatumikisha kingono watawa wa kanisa hilo na kwamba tatizo hilo limekuwa likiendelea.

Alisema kuwa mtangulizi wake Papa Benedict, alilazimika kufunga shirika la zima la watawa ambao walikuwa wakidhulumiwa kingono na makasisi.

 

Inaaminiwa kuwa hii ni mara ya kwanza Papa Francis amekiri hadharani kuhusu dhuluma za kingono dhidi ya watawa wa kanisa hilo kubwa zaidi duniani.

 

Amesema kuwa kanisa limejaribu kukabiliana na tatizo hilo na kwamba juhudi hizo bado ''zinaendelea''.

 Papa alitoa tamko hilo kwa wanahabari akiwa kwenye ziara yake kihistoria katika eneo la mashariki ya kati.

 

Alikiri kuwa makasisi na maaskofu wamekuwa wakiwanyanyasa watawa, na kwamba kanisa "linashughulikia suala hilo"

Mwezi Novemba mwaka jana kongamano la kimataifa la watawa wa kanisa katoliki duniani lililaani "utamaduni wa ukimya na usiri" ambao unawazuia kuzungumzia changamoto wanazopitia.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon