Mwandishi wa kwanza kutoka Afrika ya Mashariki aliyetunga riwaya kwa Kiingereza-Ngugi wa Thiongo,


Ngũgĩ wa Thiong'o (amezaliwa 5 Januari 1938) ni mwandishi Mkenya aliyeandika kwa Kiingereza lakini siku hizi anatumia lugha ya Gikuyu.

Maandishi yake ni pamoja na riwaya, tamthilia, hekaya, insha na uhakiki. Ameanzisha gazeti la lugha ya Gikuyu Mũtiiri.

Tangu mwaka 1982 ameishi nje ya Kenya akifundisha kwenye vyuo vikuu mbalimbali kama vile, New York na Irvine/California.

Ngugi amezaliwa Kenya katika kijiji cha Kamiriithu karibu na Limuru, wilaya ya Kiambu katika jamii ya Wagikuyu akabatizwa James Ngugi. Alikuwa mtoto wa tanowa mke wa tatu wa baba yake Thiong'o wa Nducu.

1964 akachukua nafasi ya masomo huko Chuo Kikuu cha Leeds. Hapo Uingereza alitunga riwaya ya "WEEP NOT, CHILD" (1964) akiwa mwandishi wa kwanza kutoka Afrika ya Mashariki aliyetunga riwaya kwa Kiingereza. Alisimulia hadithi ya kijana Njoroge mwenye ndoto ya kuendeleza elimu yake lakini anakwama kati ya ndoto zake na hali halisi ya maisha ya Kiafrika chini ya ukoloni.

Kazi yake ya kifasihi ilimpeleka katika mzozo na serikali. Kuanzia mwaka 1976 Ngugi alishirikiana na wanakijiji Wagikuyu karibu na Limuru kuanzisha maagizo ya tamthilia katika lugha yao.

Mwaka 1976 riwaya yake ya "PETALS OF BLOOD" ilichora picha ya watawala wapya Waafrika jinsi walivyochukua nafasi ya wakoloni wa awali wakidharau na kukandamiza wananchi. Mwaka uleule aliandika tamthilia ya "Ngaahika Ndeenda" [Nitaolewa nitakapopenda].

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu