Tetesi za soka Ulaya Jumanne 05.02.2019: Insigne, Pogba, Rashford, Hudson-Odoi

February 5, 2019

Bayern Munich itarudi na ombi la £ milioni 35 kwa winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, mwenye umri wa miaka 18, katika msimu wa joto baada ya kushindwa kumsajili mchezaji huyo wa timu ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 19 mwezi Januari.

Callum Hudson-Odoi

 

Mchezaji wa kiungo cha kati wa United Paul Pogba aliwahi kutafakari kuondoka katika klabu chini ya mkufunzi wa zamani Jose Mourinho, kwa mujibu wa kakake, Mathias.

Paul Pogba

 

Liverpool imewasilisha ombi la takriban Euro milioni 70 kwa mshambulaiji wa Napoli Lorenzo Insigne, mwenye umri wa miaka 27.

Lorenzo Insigne

 

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, anafanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya katika klabu hiyo ambayo huenda wakaongeza mshahara wake kwa mara mbili hadi zaidi ya £150,000 kwa wiki.

Marcus Rashford

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon